Sunday, July 31, 2011

RAIS DR.SHEIN AKISOMA RISALA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein, akisoma risala ya kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kuwatakia wananchi kheri kati mfungo huo kwasalama,pia kuwataka wajitahidi katika kufanya ibada kwa wingi na kuzidisha imani katika jamii.
Picha na Ramadhan Othman,IKULU.

Saturday, July 30, 2011

CCM - Kilimanjaro Yatoa Salaam Za Pole Kwa Majeruhi Wa Ajali Ya Lori na Basi iliyoua Watu 11 Nakujeruhi 26

Katibu wa mkoa wa Kilimanjaro,Steven Kazidi (kulia),akipatamaelezo kutoka kwa muuguzi mkuu wa Hospital ya Rufaa ya KCMC, Redempta Mamseri kuhusu maendeleo ya majeruhi waliolazwa katika hosiptal hiyo kufuatia ajali ya basi la LimSafari iliyotokea juzi joni nje kidogo ya manispaa ya Moshi.
katibu wa CCM mkoa wa kilimanjaro,Steven Kazidi,akimpa pole Bi.Esimend Parimina ambaye amelazwa katika Hospital ya Rufaa ya KCMC baada ya kujeruhiwa jicho lake la kulia katika ajali ya basi la Lim Safari iliyotokea juzi jioni eneo la kibosho road nje kidogo ya Manispa ya Moshi,watu 11 walipoteza maisha yao na wengine 26 kujeruhiwa vibaya.Picha na Mdau Bashir Nkromo
---
CHAMA cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Kilimanjaro,kimetoa pole kwa majeruhi wa ajali ya Basi iliyotokea juzi jioni katika bara bara ya kibosho road nje kidogo yaManispaa ya Moshi.

Katika ajali hiyo iliyohusisha basi la Lim Safari lenye namba za usajili T489BJR na roli la mizigo aina ya Bitisubishi Fuso lenye namba za usajili T884BFJ likiendeshwa na dereva wake Sifael Kaaya,watu 11 walifariki papo hapo wakiwamo madereva wote wa magari hayo mawili. Wote waliofariki ukiondoa madereva hao,ni vibarua waliokuwa wakirejea makwao

huko machame wilaya ya Hai wakitoka kuvuna kahawa katika shamba la kahawa laKilimanjaro Plantretion Ltd ambalo lipo eneo la Kibosho wilaya ya Moshi Vijijini.

Mashuda wa ajli hiyo walisema dereva wa basi hilo,alikuwa amelewa na hakuweza kusikia kilio cha abiria wake waliomtaka apunguze mwendo.
Akitoa pole jana katika Hosiptal ya rufaa ya KCMC baada ya kutembelea majeruhi

wa ajli hiyo,katibu wa CCm mkoa wa Kilimanjaro,Steven Kazidi,alisema ajali hiyoinatoa funzo kwa mamlaka husika kuwajibika katika kusimamia sheria za usalama barabarani.

Katibu huyo alisema kuwa,aajli nyingi zinatokea kutokana na uzembe wa madereva na kutaka jitihada zifanywe na vyombo husika kutoa adhabu kali kwa madereva wanaosababisha ajali.Alisema Chama cha Mapindizi CCM kimeguswa na ajali hiyo na katika kuonesha kwavitendo,CCM ilitoa msaada wa sh,600,000 na kati ya hizo sh,300,000 zilitolewa na Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Manispaa ya moshi .

Msaada huo aliutoa kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya uuguzi katika Hospital hiyo ya KCMC Redempta Mamseri aliyepokea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospital hiyo,Moshi Ntabae.

Kazidi ambaye alitembelea Idara ya upasuaji katika hospital hiyo na kuzungumza na baadhi ya majeruhi ,alifuatana na katibu wake msaidizi,Habas Mwijuki, Kamanda ya UVCCM Manispaa ya Moshi Agrrey Marealle na Katibu wa CCM Manispaa ya
Moshi,Amos Shimba.

Kwa upande wake kamanda wa UVCCM Manispaa ya Moshi,Agrrey Marealle ,alitioa wito kwa serikali kuona umhimu wa ajali za barabarani kuongezwa katika orodha ya majanga ya kitaifa pamoja na kuweka sheria kali za kudhibiti uzembe kwa
madereva.

Aidha Marealle alishauri serikali kuboresha elimu ya madereva kwa kutoa elimu kila mara juu ya sheria za usalama barabarani,kudhibiti mianya ya rushwa ikiwamo biashara ya leseni bandia na pia kuwa na utaratibu wa madereva kurudia majaribia ya udereva(driving test) mara kwa mara .

alishauri pia kuweka mkazo katika kuwadhibiti madereva wanaoendesha vyombo vya moto huku wakiwa wamelewa,kupunguza safari za usiku pamoja na kutoa muda wa kupumzika kwa madereva wa mabasi ya abiria na magari ya mizigo bila hivyo taifa litaendelea kupoteza nguvu kazi hasa vijana.

"Bila hivyo tutaendelea kupoteza watu hususani vijana ambao ndiyo raslimali kuu ya nchi,kampeni hii inahitaji ushirikiano kati ya polisi na serikali,vyama vya siasa,vyombo vya habari,madhehebu ya dini na jamii kwa ujumla"alisema Marealle.

Thursday, July 28, 2011

Kamanda wa waasi auawa Libya

Abdel Fattah Younes alimuasi Gaddafi na kujiunga na waasi
Kiongozi wa kijeshi wa waasi nchini Libya wanaokabiliana wakitaka kumpindua Kanali Muammar Gaddafi ameuawa, baraza la mpito la Libya limesema.
Kiongozi wa baraza hilo Mustafa Abdul-Jalil amesema Jenerali Abdel Fattah Younes ameuawa na watu wanaomuunga mkono Gaddafi, na kiongozi wa watu hao tayari amekamatwa.
Amesema Jenerali Younes aliitwa kwenye mkutano ambapo alitakiwa aeleze kuhusu harakati za kijeshi, lakini aliuawa kabla ya kufika kwenye kikao hicho.
Taarifa zinasema kuwa Jenerali Younes alishukiwa kuwa na uhusiano na majeshi yanayomuunga mkono Gaddafi.
Jenerali Younes ni waziri wa zamani wa mambo ya ndani ambaye alikimbia na kujiunga na upande wa upinzani mwezi Februari.
Wasaidizi wawili wa Jenerali Younes, Kanali Muhammad Khamis na Nasir al-Madhkur, pia waliuawa kwenye shambulio hilo, Bwana Jalil alisema.
Taarifa ambazo hazikuweza kuthibitishwa zilisema kuwa Jenerali Younes na wasaidizi wake wawili walikamatwa mapema siku ya Alhamisi katika eneo la kaskazini mwa Libya.
Mapema siku ya Alhamisi, waasi walisema kuwa wameteka mji muhimu wa Ghazaya karibu na mpaka wa Tunisia, baada ya makabiliano makali na vikosi vya Kanali Gaddafi.Chanzo ni bbckiswahili

Naibu Waziri wa Utamaduni Kutoka Nchini China Amtembelea Waziri Mkuu Mizengo Pinda Mjini Dodoma-Leo

Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka nchini China, Zhao Shaohua, akiangalia zawadi ya picha ya pundamilia aliyopewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinga (kushoto) wakati naibu waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma leo. Zhao pamoja na ujumbe wake wako nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua (katikati) baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa mjini Dodoma leo Kulia ni Zhao Haisheng aliyeapambana na ujumbe huo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni, Anjela Ngovi, akimvalisha kanga Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua, wakati naibu waziri huyo alipotembelea mjini Dodoma leo kwa ajili ya kuonana na viongozi wa Serikali huku waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Prof. Helmasi Mwansoko (kulia) wakishuhudia .
Naibu waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua, akiangalia ngoma ya kabila la kisukuma iliyokuwa inachezwa na kikundi cha ngoma cha Mwinamila cha mjini Dodoma baada ya Naibu Waziri huyo kuwasili mjini Dodoma leo.Picha Zote na Anna Nkinda-MAELEZO

Tuesday, July 26, 2011

Rais Jakaya Kikwete Atembelea Kituo Cha Utafiti Naliendele

Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti Dr Geofrey Mkamilo wa kituo cha Naliendele kuhusu zao la muhogo
Rais Jakaya Kikwete akiangalia chupa ya juice iliyotengenezwa na mabibo ya korosho(cashew apple)katika kituo cha Utafiti Naliendele huku Dr Peter Masawe, Mtafiti Kiongozi wa korosho nchini akimpatia maelezo ya ubora wa kinywaji hicho tarehe.

Monday, July 25, 2011

Njaa Pembe ya Afrika: Ufaransa yatahadharisha kuwa 'kashfa’


Watoto wakipatiwa msaada wa chakula Mogadishu
Dunia ‘imeshindwa kuhakikisha kuna chakula cha kutosha’, Waziri wa Kilimo wa Ufaransa amesema katika mkutano msaada wa chakula.
Mkutano huo ni wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Chakula unaojadili ukame katika eneo la Mashariki na Pembe ya Afrika.
"Kama hatutachukua hatua madhubuti, njaa itakuwa kashfa ya karne hii." Shirika la Habari za AFP limemnukuu Bruno Le Maire akizungumza mjini Rome.
Zaidi ya watu milioni 10 inakadiriwa kuwa wako katika hali ya hatari ya ukosefu mkubwa wa chakula na baa la njaa limetangazwa katika maeneo mawili nchini Somalia.
Mbele ya mkutano huo, Benki ya Dunia imeahidi msaada wa dola milioni 500 (£307milioni).
Kiasi cha dola 12milioni kitapelekwa mara moja kusaidia waloathirika zaidi na kile Umoja wa Mataifa unakiita Ukame mbaya zaidi kutokea eneo la Afrika ya Mashariki katika miaka 60.
Lakini kiasi kikubwa cha fedha kitaelekezwa katika miradi ya muda mrefu ya kuwasaidia wakulima na pia wafugaji.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa mataifa wafadhili kutoa pesa zaidi za msaada kiasi cha dola 1.6
Awali shirika la Msalaba Mwekundu limesema limegawa chakula katika maeneo yaliyoathirika zaidi yanayodhibitiwa na makundi ya wapiganaji wa kiislam.
Wakifanya kazi kwa kupitia kamati ya wenyeji, Shirika la Msalaba Mwekundu limegawa chakula kwa watu 24,000 kwa lori.

'Ni suala la kufa na kupona'

Kuna mashirika mengi ya misaada ya ndani ambayo tayari yanafanya kazi nchini kote Somalia-ukweli kwamba mara nyingi unapotelea kwenye usumbufu wa al-Shabaab juu ya mtazamo wa kikatili unaoelekezwa kwa mashirika makubwa WFP.
Hakuna mashaka kuwa ukame, na harakati za mageuzi kwa nchi za Kiarabu yametikisa hali ya usalama nchini Somalia.
Ushahidi usiothibitishwa unaonyesha kuwa al-Shabab sasa wameishiwa fedha, wamegawanyika zaidi na wapiganaji wengi wa jihadi kutoka nje waliokuja kujiunga nao wameondoka kwenda kujiunga na makundi mengine.
Al-Shabab, kundi linalohusishwa na al-Qaeda linadhibiti sehemu kubwa ya maeneo ya Kusini na Kati nchini Somalia, liliweka amri ya kuzuia mashirika ya misaada ya kigeni katika maeneo yake mwaka 2009, katika kwa sasa limeruhusu kwa sehemu misaada itolewe.
Lakini WFP linasema bado haliwezi kuwafikia watu wapatao milioni 2.2 ndani ya Somalia huku wakimbizi wakiendelea kumiminika kwenye mipaka ya nchi za Kenya na Ethiopia.
Somalia inaripotiwa kuathirika zaidi na upungufu mkubwa wa chakula, lakini Kenya na Ethiopia pia zimeathiriwa.
Wachambuzi wanasema ukame umesababishwa na upungufu wa mvua na kushindwa kwa serikali kuiwesha miradi ya kilimo na umwagiliaji kifedha
Mkutano wa mawaziri kutoka mataifa ya G20 katika makao makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa mjini Roma liliombwa na Ufaransa, mwenyekiti wa sasa wa Kundi la G20 lenye nguvu Kiuchumi.
"Mkutano wetu ni suala la kufa na kupona kwa makumi ya maelfu ya watu ," Bw Le Maire alisema wakati mkutano huo ulipofunguliwa, kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la AFP.
Bob Geldof na wanaharakati wengine mashuhuri wanatoia wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa pesa zaidi za msaada.
Wanazishutumu nchi kama Italia, Ufaransa, Mataifa ya Kiarabu na Ujerumani kuwa kuchangia kidogo sana ikilinganishwa na utajiri zilizo nao.

Hatua za tahadhari Ethiopia

Bw Le Maire ameimbia BBC kuwa lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuratibu msaada na kukabiliana na baa hilo.
"Lengo la pili ni kutafakari kuhusu za siku za usoni na mtazamo wa muda mrefu kwa sababu tunachokiona Afrika ni kwamba watu wanahitaji kuwa a chakula chao wenyewe na kuwa na kilimo chao" alisema.
Mchambuzi wa BBC Afrika Martin Plaut anasema watu wengi walio katiakti mwa janga hili huko Ethiopia wamejitokeza lakini hawajasikiwa.
Hii ni kutokana na serikali ya Addis Ababa ina mpango kamambe wa kuchukua tahadhari, anasema.
Kujipanga mapema kwa tahadhari kuna maana kuwa utawala Ethiopia unaweza kuidhibiti mapema mara noja ukame unapojitokeza zaidi.
Ugawaji wa chakula wa kwanza ulianza mwezi February na umeendelea katika maeneo yaliyoathirika zaidi katika ukanda huo.
Jamii zinapata shida, lakini njaa iliyoikumba nchi jirani ya Somalia, Ethiopia wameiepuka na mfumo wa kudhibiti majanga uliowengwa tangu mwaka 1980s umefanya kazi.Chanzo ni bbckiswahili

Sunday, July 24, 2011

Zeco:Wazungumzia Kuhusu Matumizi Ya Majenereta Ya Dharura

MENEJA Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Mbarouk akizungumza na Waandishi wa habari vyombo mbalimbali, Ofisini kwake kuhusiana matumizi ya majenereta ya dharura.
WAANDISHI wa habari wakimsikiliza Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme alipokuwa akitowa maelezo ya mwenendo wa matumizi ya Umeme kwa Wateja wa bidhaa hiyo ofisini kwake Golioni.Picha na Mdau Othman Maulid-Zanzibar

RATIBA YA FUTARI YA PAMOJA WASHIGTON DC

RATIBA YA FUTARI YA PAMOJA WASHINTON DC
www.tamcousa.org

Assalam Alaykum,

Ndugu waislamu Uongozi wa Tanzanian Muslim Community in Washngton DC
Metro(TAMCO) unawakaribisha na kuwajulisha kuwa kama kwaida yetu kwa mwezi
wa Ramadhani tutakuwa tukifuturu pamoja jumammosi na jumapili zote za Mwezi wa
Ramadhani.

Tunaombwa tuudhurie na tuwajulishe wengine wote:

SAT. 08/06/11 – Sligo Avenue Neighborhood Park

Adress:
500 Sligo Avenue, Silver Spring, MD 20910

XXXXXXXX

SUN.08/07/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park
SAT.08/13/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park
SUN.08/14/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park
SAT.08/20/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park
SUN.08/21/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park
SAT.08/27/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park
SUN.08/28/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park

Address:
Hillandale PAB - Hillandale Local Park:
10615 New Hampshire Avenue,
Silver Spring,
MD 20903

XXXXXXX
TAMCO EID DAY: SAT. 09/05/11 – Hillandale Local Park

Starting at 4.00PM

If you experience problems locating the address,
Please contact TAMCO Leadership.
At
uongozi@tamcousa.org OR

Tamcotuwasiliane-owner@yahoogroups.com

Wenu
Mwenyekiti
Iddi Sandaly

Thursday, July 21, 2011

Tanzania Na Afrika Kusini Zatiliana Saini Mkataba Wa Ushirikiano Kiutamaduni

Waziri wa Habari,Utamaduni na michezo Dr.Emmanuel Nchimbi na Mwenyeji wake Waziri wa Utamaduni wa Afrika ya Kusini Paul Mashatile wakisaini mkataba wa kuanzishwa rasmi ushirikiano katika Nyanja ya utamaduni kati ya Afrika ya kusini na Tanzania jana jijini Pretoria huku Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Afrika ya kusini Jackob Zuma wakishuhudia...



Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika viwanja vya kumbukumbu ya mshujaa waliopigania uhuru wa Afrika ya Kusini nje kidogo ya jiji la Pretoria jana. Wapili kushoto ni Mama Salma Kikwete na watatu kulia ni mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini.Rais Kikwete yupo nchini Afrika ya Kusini kwa Ziara rasmi ya Kitaifa ya Siku mbili...

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini wakigonga glasi wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Zuma kwa heshima yake wakati wa kilele cha Ziara Rasmi ya siku mbili nchini humo(Picha Zote; Freddy Maro)

MKUU WA MKOA WA MBEYA AKUTANA NA MADEREVA TUNDUMA(BODA) KUZUNGUMZIA KUONGEZEKA KWA SIKU ZA KUSIMAMIA MAGARI MIZANI KUTOKA SIKU TANO HADI SABA

Mkuu wa mkoa wa Mbeya akifafanua jambo kwenye mkutano huo na madereva
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mwakipesile akiwa amekasirika baada ya kukutana na maswali mengine yanayoonyesha kutokukubaliana na yale wanayoshauriwa!
Uongozi wa madereva pamoja na mkuu wa mkoa katikati na kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Mbozi wakisikiliza jambo kutoka kwa madereva hao
Meneja wa TRA kitengo cha forodha bwana Rogacian Shirima akizungumzia kuongeza idadi ya siku za kusimamia magari hayo kutoka Dar hadi Tunduma ama Kasumulu ambapo watachukua siku saba badala ya siku tano za awali.
Kamanda wa polisi wilaya ya Mbozi Afande Ernest Dudu akizungumzia utaratibu Trafiki kukagua magari hayo tu pale yanapokuwa mizani.
Hapa viongozi wa madereva wa Magari ya biashara wakikataa hivi hivi pale hoja yao ilipokumbana na upinzani wa wale wanaowaongoza.Chanzo ni mbeyayetu.blogspot.com

Wednesday, July 20, 2011

zinduzi wa Tamasha La Mzanzibari Lafana

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed akizinduwa Tamasha hilo la 17 la Mzanzibar kwa kupiga bastola kuashiria kuazisha resi za ngalawa.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud akitowa hutuba ya Ufufunguzi wa Tamasha la 17 la Mzanzibar lililofanyika katika Ufukwe wa Pwani ya Nungwi.
WASANII wa Oman wakifuatilia maonesho ya tamasha la Mzanzibar, nao walialikwa kuonesha ngoma za Utamaduni wa kwao.
KIKUNDI cha Taarab cha Sanaa wakiimba wimbo maalum wa Zinduzi wa Tamasha.Picha na Mdau Othman Maulid Othman-Zanzibar

Tuesday, July 19, 2011

Waziri Wa Maliasili Na Utalii Azindua Vodacom Foundation’s Serengeti Wild Dogs Conservation Project).


Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare akimkabidhi sanamu ya mbwa mwitu Mkurugenzi wa shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA Allan Kijazi kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mradi wa utunzwaji wa mbwa mwitu katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti(Vodacom Foundation’s Serengeti Wild Dogs Conservation Project).Mradi huo ulizinduliwa juzi na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige(katikati)ambapo Vodacom Foundation imetoa dola za Kimarekani 450,000 kwa miaka mitatu.


Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare(kulia)akimuonyesha kitu Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bi Mwamvita Makamba kwenye kambi ya utalii ya Soroi, Serengeti wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuhifadhi mbwa mwitu (Vodacom Foundation’s Serengeti Wild Dogs Conservation Project) katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
--------
Na Mwandishi wetu,Serengeti.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige,juzi amezindua mradi wa uhifadhi Mbwa Mwitu ujulikanao kama “Vodacom Foundation Serengeti Serengeti Wild Dogs Conservation Project” katika hifadhi ya taifa ya Serengeti,mradi ambao unafadhiliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa kiasi cha dola zakimarekani 450,000 kwa miaka mitatu.

Akizungumza katika uzinduzi wa Mradi huo,Waziri Maige alisema Mbwa mwitu ni miongoni mwa wanyamapori ambao wapo hatarini kutoweka duniani hivyo jitihada kubwa zinahitajika kuwalinda na kuwahifadhi.Waziri Maige alisema katika bara la Afrika kuna idadi ya Mbwamwitu, wanaofikia 8000 na Tanzania pekee ina jumla ya mbwamwitu 3500 ambao wapo hatarini kutoweka hivi sasa.

Alisema katika hifadhi ya Serengeti makundi ya Mbwamitu ambayo yalikuwa yanaonekana sasa yametoweka na mara ya mwisho mbwamwitu wawili tu walionekana mwaka 1998.

Waziri Maige alisema, Mwa mwitu hao, wamekuwa wakitoweka kutokana na kuuwa na wananchi baada ya kula mifugo yao, kuugua magonjwa mbali mbali ikiwepo kichaa cha mbwa.

“napenda kuwapongeza Vodacom kwa kujitokeza kudhamini uhifadhi wa mbwamwitu kwani wanasaidia kuvutia watalii kuja Tanzania na hivyo kuongeza pato la taifa”alisema Maige.

Alisema sekta ya utalii nchini inachangia asilimia 17 ya pato la taifa hivyo ni wajibu wa makampuni kusaidia sekta hii kwani imeajiri zaidi ya watu 700,000 ambao pia ni wateja wa kampuni mbali mbali.Awali Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania Dietlof Mare.alisema kampuni hiyo, imeamua kujitokeza na kusaidia sekta ya utalii ili kuongeza pato la taifa.

Alisema Vodacom inaamini kuwa Tanzania ni nchi ya kipekee duniani katika sekta ya utalii kutokana na kuwa na vivutio vingi na hivyo lazima vitunze na kuhifadhiwa.

“vodacom tumeamua kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano kusaidia sekta ya utalii na tunaamini katika ufadhili wetu, mbwamwitu waliohatarini kutoweka sasa watarejea hifadhi ya Serengeti”alisema Mare

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori,(TAWIRI) Dk.Simon Mduma alisema TAWIRI ambao ndio wasimamizi wa mradi huo watahakikisha wanashirikisha jamii kuwalinda na kuwahifadhi Mbwa mwitu.

Mduma alisema katika siku za karibu makundi ya Mbwamwitu yamekuwa yakionekana katika pori tengefu la Lolindo na vijiji vya Tarafa ya sale ikiwepo Samunge na tayari umewekwa utaratibu wa kuwafuatilia na kuwalinda.

Dk Willbrod Slaa:Tumeunda Tume Kumhoji Mbunge wa Maswa Magharibi{Chadema}John Shibuda

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa
Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda
-----

Na Geofrey Nyang'oro
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeunda tume itakayoongozwa na Profesa Abdallah Safari kumhoji Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu zinazomkabili.

Hii ni mara ya pili kwa Shibuda kuhojiwa na jopo maalumu la Chadema kwani tayari aliwahi kuhojiwa baada ya kupingana na msimamo wa chama hicho wa kumsusia Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akizundua Bunge Desemba mwaka jana kwa kuhudhuria dhifa katika Ikulu ya Chamwino huku akiweka bayana kupingana na msimamo huo.

Mapema mwezi huu alitoa tena kauli ambazo Chadema imeziita ni zenye kukiuka maadili hali iliyomfanya Mkurugenzi wake wa Mambo ya Nje, John Mnyika kuwasilisha malalamiko rasmi ndani ya Kamati Kuu (CC).

Akizungumza Dares Salaam jana baada ya kikao cha CC, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa alisema hatua ya kuunda tume kwa ajili kufanya kazi ya kupitia tuhuma hizo imetokana na madai ya mlalamikaji kuwa na mantiki.

Wajumbe wengine wanaounda kamati hiyo ni Edson Mbogoro, Said Mzee, Lazaro Masey na Ester Daffi ambaye si mjumbe wa kamati, bali atafanya kazi kama mratibu wa kamati hiyo akitokea Ofisi ya Katibu Mkuu.

Dk Slaa alisema: “Kikao cha kamati kilichokaa jana (Juzi) hakikujadili suala la Shibuda na mambo yaliyopo bungeni, bali kilipokea taarifa ya malalamiko kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu juu ya kitendo cha Shibuda kukiuka maadili. Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema ili hatua ziweze kuchukuliwa kwanza ni lazima malalamiko yawasilishwe Ofisi ya Katibu Mkuu wa chama naye kuyawasilisha kwenye Mkutano wa Kamati Kuu.”