Wednesday, September 14, 2011

HIVI NDIVYO NDEGE ILIVYO UMIA BAADA YA KUANGUKA ENEO LA NANE NANE UYOLE MBEYA



HABARI KAMILI 
Ajali ya ndege namba  9J-BIO SESINA 206, imetokea leo asubuhi majira ya saa tatu eneo la Nanenane Uyole jijini Mbeya  na abiria wanne wanusurika kifo na hakuna aliyefariki.

Abiria walionusurika kifo ni pamoja JVER WAAK Umri wa Miaka 49 ambayealikuwa Rubani, Raia wa Afrika Kusini, Bwana CHRISTIAN BASIL MMASI umri miaka 30, Ambaye ni Afisa Utawala wa mashamba ya Kapunga wilaya ya Mbarali, Balozi MOHAMMED RAMIA kabula leke ni Mmakua mwenye umri wa miaka 64, mkazi wa Masaki jijini Dar es Salaam ambaye ni mfanyakazi EXPORT TRADING na Bwana SUNNY TAYIR mwenye umri wa miaka 50 ambaye ni Mhindi na ni mfanyakazi wa EXPORT TRADING.

Na chanzo cha ajali hiyo akijafahamiaka mpaka sasa.

Imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Bwana ANACLET MALIMBISA
 NDEGE INAVYO ONEKANA BAADA YA KUPATA AJALI...

  BAADHI YA WATU WALIO  FIKA ENEO HILO LA TUKIO KUTOA MSAADA BAADA YA AJALI HIYO.

PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG

Sunday, September 11, 2011

Saidiazanzibar - We need your help


PRESS RELEASE

On Friday 10th September 2011, the ferry M.V. Spice Islander, travelling between Dar es Salaam, Zanzibar, Pemba and Tanga, capsized in deep waters in the Pemba Channel, north of Zanzibar island. 

The true numbers of those injured or dead in the tragedy has yet to be established, but it is now acknowledged that there were many more passengers than the 610 listed on the ship manifest. As of Saturday night, 200 are dead, 500 have been rescued and many are still missing. The full extent of the tragedy will not be known for several more days. 

Saidia Zanzibar (www.saidiazanzibar.org) is an emergency fundraising website, to provide caring members of the public, in Zanzibar and the world at large, with a framework to commit some of their time and money for the assistance of those tragically affected by the disaster.

We will be posting updates in the coming days, including a Zanzibar bank account to which money can be sent, and details of those organizations to whom the money will be subsequently disbursed on your behalf. 

The fundraising effort will be overseen by the Zanzibar Association of Tourism Investors (www.zati.org), a registered NGO, who will co-ordinate donations and offers of assistance from their office located in the Cine Afrique in Malindi, Stone Town, Zanzibar.

Further updates will be posted throughout the period starting 12th September 2011. Email enquiries can be sent to saidia@saidiazanzibar.org.

Zitto Kabwe Anaelezea Hisia Zake Juu Ya Msiba Mkubwa Wa Kitaifa

|
Taifa Msibani, Umoja wetu na Utu wetu Shakani
by Zitto Z Kabwe on Sunday, 11 September 2011 at 16:19

(Nimeandika makala hii nikiwa katika Benchi la Hospitali ya Mnazi

Mmoja hapa Zanzibar. Mniwie radhi kama kuna spelling mistakes kwani
nilitaka hisia zangu ziwe as raw as possible - Zitto Zitto and not
Zitto a Politician).

Jana asubuhi tarehe 10 Septemba 2011 Taifa liligubikwa na habari za

kushtusha za maafa. Mwanzoni taarifa zilisambaa kwamba zaidi ya watu
2000 walikuwa kwenye Boti MV Spice Islander lililopinduka na kuzama
mbele kidogo ya Nungwi likielekea kisiwani Pemba. Habari hazikuwa za
uhakika sana kwani vyombo vyetu vya habari na hasa Televeshini ya
Taifa havikuwa vikitoa habari juu ya ajali hii.

Habari zilisambaa kupitia mitandao ya intaneti na kufuatia uchu wa

habari nilianzisha #ZanzibarBoatAccident katika mtandao wa twitter ili
tuweze kufuatilia kwa karibu habari zote za ajali hii.

Habari zilisambaa kuwa Televisheni ya Taifa ilikuwa inaonyesha muziki

wa Taarab na Baadaye vipindi vingine vya kawaida bila kutoa habari kwa
Umma kuhusu msiba huu.

Watanzania waliokoa wakiwasiliana kupitia twitter na facebook walikuwa

na hasira sana na kituo cha TBC1 kutoonyesha au kupasha habari juu ya
ajali hii. Mpaka saa moja jioni kituo hiki cha Televisheni ya Taifa
kilikuwa kinaonyesha watu wakicheza muziki wa Kongo, wanawake
wakikatika viuno na hata ngoma za asili.

'Hallo, washa TBC1 uone Televisheni yenu inachoonyesha' yalikuwa ni

maneno ya Mwakilishi Ismael Jussa Ladhu aliponipigia kuonyesha
kusikitishwa kwake na kituo hiki. Mpaka jioni tulikuwa tumepata
taarifa kuwa Watanzania wenzetu 198 walikuwa wamepoteza maisha. 570
hivi walikuwa wameokolewa.

Binafsi nilipotembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja niliweza kumwona Binti

aliyeitwa Leyla, akisoma darasa la Nne huko kisiwani Pemba. Leyla
alipona, aliokolewa. Nilimwambia leyla atapona na kurudi Shuleni.
Mpaka ninapoandika tumeambiwa kuwa Watanzania 240 wamegundulika
kupoteza maisha na zaidi ya 600 wameokolewa.

Napenda kuwapongeza sana waokoaji wetu, wavuvi wa kijiji cha Nungwi na

vijiji jirani, wamiliki wa mahoteli waliojitolea vifaa vyao kwenda
kuokoa watu na wanajeshi wetu wa majeshi ya ulinzi na usalama kwa kazi
hii kubwa ya kuokoa. Kwa kweli tumeokoa watu wengi kuliko
ilivyotarajiwa. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejitahidi sana,
ilitulia na kuonyesha uongozi thabiti katika juhudi za uokoaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akafuta ziara yake huko

Canada, ziara iliyokuwa imeandaliwa muda mrefu na kwa gharama. Lakini
Rais aliona ni vema kupata hasara kuliko kuwa nje ya Nchi kipindi
hiki. Hakutaka hata kumtuma Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Alifuta.
Akatangaza siku 3 za kuomboleza.

Hata hivyo waandaaji wa Miss Tanzania waliona hasara kubwa kuahirisha

shindano la Urembo usiku huo. Wangepata hasara! Hata wafadhili wao
Kampuni ya simu za mkononi ya vodacom ambao miongoni mwa waliofariki
wamo wateja wa vodacom, waliendelea na shindano hili.

Jumatatu, tarehe 12 Septemba 2011 ni siku ya khitma ya kuwaombea marehemu wetu.


Nimeamua kutotumia simu yangu ya Voda kwa siku nzima, sina njia ya

kuiadhibu Kampuni hii isipokuwa kugoma kutumia simu yao japo kwa siku
moja kuonyesha kutoridhishwa kwangu na uamuzi wao wa kutojali msiba
huu kwa Taifa.

Misiba huweka jamii pamoja. Msiba huu uliotokea Zanzibar ni jaribio

kubwa kwa Umoja wa Taifa letu. Shirika la Utangazaji la Taifa
limeshindwa jaribio hili la kudhihirisha Umoja wetu katika kipindi
hiki. Nataraji wakubwa wa Shirika hili linaloendeshwa kwa kodi
watawajibika au kuwajibishwa!

Jumla ya Majeruhi na marehemu sasa inafikia zaidi ya Abiria 800!

Asubuhi ya jana 10 Septemba 2011 tuliambiwa na Serikali kwamba uwezo
wa Boti la MV Spice Islander ilikuwa ni abiria 500 na wafanyakazi 12.
Pia tumejulishwa kuwa boti hili lilikuwa la Mizigo na sio la Abiria.

Natumai mara baada ya kumaliza maombolezo haya ya siku tatu Wakuu wa

Mamlaka zinazohusika na usafiri wa Majini wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar watawajibika au kuwajibishwa. Mkuu wa Bandari ya Zanzibar
Mustafa Aboud Jumbe na Waziri wa Miundombinu Hamad Masoud wanapaswa
kufukuzwa kazi mara moja kama hawatawajibika wenyewe kwa kujiuzulu.

Kufukuzwa kwao kazi hakutarudisha ndugu zetu duniani bali itakuwa ni

somo kuwa hatutarudia tena kufanya makosa yaliyoleteleza ajali kama
hii.

Mwenyezi Mungu atupe subira wakati huu wa msiba mkubwa katika Taifa

letu. Alaze roho za marehemu wetu mahala pema peponi na awape unafuu
wa haraka majeruhi wetu.

Zitto Kabwe, Mb

Saturday, September 10, 2011

Ahadi Ya Ngeleja Yaongeza Machungu Mgawo Wa Umeme

MATUMAINI yaliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kwamba makali ya mgawo wa umeme yangepungua kwa kiasi kikubwa kuanzia Septemba 7, mwaka huu yamekuwa kinyume chake kutokana na adha ya upatikanaji wa nishati hiyo kuongezeka.

Maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam hayana umeme yapata siku tatu sasa, huku mengine yakipata nishati hiyo mara moja katika muda wa saa 36 na 48.
Ngeleja alitoa ahadi kwamba kungekuwa na nafuu ya mgawo baada ya kuwashwa kwa mitambo ya umeme ya Kampuni ya Symbion na ile ya Aggreko ambayo kwa ujumla wake, ilitarajiwa kuzalisha megawati 137.5.
Hata hivyo, hadi jana jioni mitambo hiyo haikuwa imewashwa hivyo kusababisha maeneo mengi ya Dar es Salaam kuendelea kuwa gizani.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili jana umebaini kuwa baadhi ya maeneo ya yakiwamo Ubungo, Mwenge, Kimara, Temeke, Keko na Sinza makali ya mgawo wa umeme yamezidi huku Tabata kukiwa hakuna umeme kwa siku tatu mfululizo.
Mtendaji  Mkuu wa Symbion, Stanley Munai alisema bado hawajaanza uzalishaji licha ua mafuta ya kuwashia mitambo kufika akisema kwanza wameyapeleka kuyapima ili kujua kama yanafaa ama la... “Tunasubiri majibu ili kuona kama yanafaa au hayafai.”

Alisema uamuzi wa kuyapima mafuta hayo umezingatia kwamba mtambo wao utakuwa ukiyatumia kwa mara ya kwanza, hivyo ni lazima yapimwe ili yasije kusababisha tatizo jingine.
“Ukiwasha bila kupima mafuta unaweza kuua mtambo, mafuta huwa tunachukulia katika kampuni ya kuuza mafuta ya BP,” alisema Munai.

Alipoulizwa ni lini mitambo hiyo itawashwa, Munai alisema: “ Muda wowote tu tukishapata majibu, mafuta huwa yanapimwa na kampuni ya SGS au Intertake.”

Alichoahidi Ngeleja Septemba 4
Septemba 4, mwaka huu alipotembelea mitambo hiyo iliyopo Ubungo, Ngeleja alisema makali ya umeme yangepungua kwa kiasi kikubwa akirejea ahadi aliyopewa na Symbion kwamba mitambo yao ingewashwa katika muda huo.
Ngeleja kwa kauli ya kujiamini alikwenda mbali zaidi huku akisisitiza kwamba mpaka kufikia Desemba mwaka huu, uzalishaji wa umeme utafikia megawati 572, hivyo kutamaliza kabisa mgawo wa umeme.

 “Mitambo ya Symbion ina uwezo  wa kuzalisha megawati 112 ambayo inatumia gesi na mafuta mepesi, mpaka sasa inazalisha megawati 75 tu, megawati nyingine 35.7 za mtambo huu zitaanza kuzalishwa kesho (Septemba 6) au keshokutwa (Septemba 7) baada ya kuwasili kwa mafuta mepesi” alisema Ngeleja.

Alisema kuwa mitambo ya Aggreko ambayo inazalisha megawati 100 utawashwa baada ya kukamilika kwa ufungaji wa baadhi ya vifaa zikiwemo transfoma.
Hii si mara ya kwanza kwa Ngeleja kutoa kauli kama hiyo kwani amekuwa akifanya hivyo na kutoa ahadi ambazo utekelezaji wake umekuwa mgumu.

Mapema mwaka huu, wakati akiapishwa kushika nafasi yake ya Waziri wa Nishati na Madini kwa kipindi kingine, aliutangazia umma kwamba mgawo wa umeme ungekuwa historia lakini wiki hiyo ya kwanza tangu kuapishwa kwake nchi ikatikiswa na mgawo mkubwa.

Alipotafutwa kwa ajili ya kuzungumzia ongezeko la makali ya mgawo, Meneja Uhusiano wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), Badra Masoud hakupatikana kwani simu yake ilikuwa ikiita bila majibu ya kupokewa.

Hata hivyo, mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa kuwa si msemaji wa alisema Badra alikuwa msibani na kwamba hayupo ofisini mpaka Jumatatu ijayo.

“Badra amefiwa hayupo kwa sasa, ila kuhusu suala la mtambo wa Symbion ungekwenda kuzungumza na haohao Symbion kwa sababu wao wanawauzia umeme Tanesco,” alisema mfanyakazi huyo.

Kuhusu mitambo ya Aggreko alisema mitambo hiyo itawashwa mwezi huu baada ya kukamilika ufundi.
“Unajua kuna upungufu wa megawati 300 katika Gridi ya Taifa kwa hiyo hata zikiwashwa hizo megawati 37.5 za Symbion na megawati 100 za Aggreko bado kutakuwa na mgawo, Waziri Ngeleja alifafanua kuwa mpaka Desemba mwaka huu ndipo mgawo utakwisha kabisa,” alisema mtumishi huyo.

Friday, September 9, 2011

TEMEKE KINONDONI NANI ZAIDI KATIKA MASUMBWI

Na Mwandishi Wetu Kambi ya Ilala

MABONDIA Mbwana Matumla wa Temeke na Francis Miyeyusho wa Kinondoni Dar es Salaam wanatarajia kupanda ulingoni katika pambano la kudhihirishiana ubabe kati ya mabondia wa Temeke na Kinondoni litakalofanyika Oktoba 30 mwaka huu.

Pambano hilo pia litafuatiwa na lingine kati ya Ramadhani Shauri wa Kinondoni dhidi ya Issa Sewe wa Temeke ambapo yote yatafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha Msaidizi wa Kambi ya Kinyogoli Foundation ya Dar es Salaam, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema mapambano hayo yameandaliwa na Promota Mohamedi Bawaziri kuhamashisha mchezo huo.

"Mabondia wote wameanza mazoezi na kwa upande wa Temeke wapo kambini chini ya Kinyogori Foundation chini ya kocha Habibu Kinyogori akishirikiana na mimi na tunawaandaa kucheza ngumi za kisasa sio kurusha ngumi bila mpangilio.," alitamba Super D

Alisema pambano kati ya Matumla na Miyeyusho litakuwa  la uzani wa Bantam Weight kilogramu 54 ambapo Shauri na Sewe watacheza kilogramu 58, uzito mwepesi (Light Weight).

Alisema licha ya kuhamasisha, kumekuwepo na tambo za mda mrefu kati ya mabondia wa Kinondoni, na wenzao wa Temeke ambapo mashabiki watajionea mapambano hayo.

Kocha huyo alisema mapambano hayo yatasindikizwa na mengine kutoka kwa mabondia wa Temeke na Kinondoni ambapo pia kutakuwepo na burudani mbalimbali zitakazotangazwa baadae.

--
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, September 7, 2011

Mchezaji Nazir Khalfan Atinga Ikulu Kumshukuru Rais Jakaya Kikwete na Kumkabidhi Jezi


 Mtanzania anaecheza Soko la Kulipwa katika timu ya White Caps ya Jijini Vancour Canada Nizar Khalfan akimkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Jakaya Kikwete jezi ya timu anayoichezea wakati alipokwenda kumsalimu na Kumshukuru Rais Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar Es Salaam.Picha na Freddy Maro-IKULU